ACHANA na comeback ya Newcastle dhidi ya Arsenal ile tarehe 5 Februari mwaka 2011 pale St James Park maarufu kama Sport Direct Arena kwa kipindi kile, iliyomnyanyua Rais Jakaya Mrisho Jakaya Kikwete. Rest in Peace Cheick Tiote.


Mtafute shabiki yeyote wa FC Bayern ambaye ni mzee wa leo, kijana wa jana, akupe maelezo yaliyonyooka vizuri akikuelezea ni namna gani alijisikia baada ya kufa pale Camp Nou ule usiku wa 1999.

Habari za Teddy Sheringham na Ole Gunnar Solakjaer, super sub mwenye sura ya mtoto mchanga zitarudi upya kwenye kichwa chake, huenda ndio ilikuwa ni siku yake ya kwanza kuuchukia usiku wa Ulaya. Bayern anakufa 2-1, Man United anabeba ubingwa wa Ulaya.

Sio Andrey Shevchenko, Paulo Maldini wala pacha wake mwenye sura ya upole na roho ya kikatili, Alesandro Nesta ambao waliamini macho yao ule mwaka 2004 ambapo Deportivo La Coruna walipiga comeback ya kibabe na kupindua matokeo yalikuwa yakisomeka kwa 3-0 pale San Siro na kuja kuibuka na ushindi mzito wa 4-0.


Nitakushangaa sana kama utakuwa msahaulifu kuhusu yale yaliyotokea pale Ataturk Stadium tarehe 25 mwezi Mei 2005, Liverpool wakiwa chini ya nahodha mdogo tu mwenye umri wa miaka 23 mwenye roho ya chui, walifanya jambo pale.

Walikuwa ni AC Milan walioamini kuwa kombe litakwenda San Siro mapaka kipindi cha kwanza kinakwisha, Milan walikuwa wanaongoza mabao 3-0. Kwa nini wasijiamini? Niulize kiichotokea baada ya mchezo ni kuwa Liverpool walirudi Anfield wakiwa wameshaongeza kombe la Tano la UEFA kwenye kabati.

John Terry anajiuliza ni kati ya mvua au yeye ambaye aliinyima Chelsea ubingwa wa UEFA 2008 pale Moscow dhidi ya Manchester United, au Bayern watasemaje kuhusu kuongoza mpaka dakika ya 88 mwisho wa siku ubingwa kwenda Chelsea msimu wa 2012.

Lionel Messi ana kumbukumbu nyingi sana juu ya usiku wa Ulaya, moja wapo ni kuchukua UEFA 4 akiwa na Barcelona, hawezi kuisahau comeback ya kibabe dhidi ya PSG 6-1 pale Camp Nou 2017. Ambapo aliishuhudia klabu yake ikitoka hatua ya robo fainali kwa uchawi uliokuwa kwwnye miguu ya Paulo Dybala.

Unamkumbuka Kostantinos Manolas? Huwezi kumsahau kama wewe ni shabiki wa Barca, ni mgiriki mmoja, ana roho chafu sana, aliwaua Barca dakika za kula daku, Aggregate ikasoma 4-4, Barca nje!

The Corner is taken quickly, Origiiii! Alikuwa ni Trent Arnold kijana mdogo tu wa miaka 20 aliyeisafirisha kona iliyozaa bao la 4 na kuiondoa Barcelona kwa aggregate ya 4-3, pengine Barca hawakujua ile ni Anfield, nyumba ya vichaa na walevi wenye mizuka.

Wengi sana watachukia sana kwa nini paragraph nyingine inaizungumzia tena Barcelona, ila imejileta yenyewe tu. Ila Barca watakuwa wanajiuliza, huyu bundi aliye upande wao haoni kwingine? Anaendelea kuwatengenezea mikosi na kusababisha wawe waoga wa usiku wa Ulaya.

Hivi ndivyo ninavyopata hisia ninavyoisikia ile ngoma ya UEFA, ninakumbuka mengi, nilishawahi kukaa wiki nawaza kipigo, sijui walikuwa ni Barca wale? Ila Estadio da Luz inawakumbusha nini wale Barcelona?


Watu wengi wanateseka kwenye usiku wa Ulaya kutokana na vipigo vinavyoshangaza watu kwenye UEFA champions league tangu imeanzishwa.

Unakumbuka kipigo cha Arsenal dhidi ya Bayern Munich? Unakumbuka zile goli tano pale Allianz Arena? Unakumbuka zile goli tano pale Emirates stadium wakati wanashika mitutu wakiwa chini ya kocha na mtaalamu wa mpira Arsene Wenger ? 

Arsenal walitawaliwa kwenye kila na Bayern Munich,walikosa nguvu ya kufanya kitu ambacho mashabiki walitaka wafanye.

Kitu pekee ambacho arsenal waliweza kufanya ni kutoa machozi kwanzia kwa mashabiki, wachezaji mpaka kwa viongozi 

Inawezekana Stan Kreonke kichwa kinamuuma hajui kitu gani anaweza kufanya ili kutawala soka la ulaya, Kwa bahati mbaya hata msimu huu wamatoka sare ya magoli mawili kwa mawili na mchezo wa marudiano ndio utaamua arsenal anaenda hatua nyingine au hauendi ,kibaya zaidi wanaenda kukutana na Bayern Munich yenye Harry Kane ndani yake wakati huo Kane akiwa na record nzuri ya kuifunga Arsenal .

Kane amekutana na Arsenal mara 17 tangu akiwa Tottenham Hotspur na amefanikiwa kufunga magoli 15 na tarehe 17 atakuwa pale Allianz Arena kuikaribisha Arsenal.


Mechi za UEFA champions hazijawahi kuacha kuwatoa watu macho, unanikumbuka ile come back ya Real Madrid dhidi ya Manchester City pale Santiago Bernabeu wakati Rogrido Goes anatoka benchi na kwenda kufunga goli la kuipeleka Real Madrid Nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya? Najua yote unayakumbuka kwa bahati nzuri tutaenda kushuhudia tena mtanange huu mkali wa kuwatunisha Manchester City dhidi ya Real Madrid pale Bernabeu na ukumbuke mchezo wa kwanza ulitamatika kwa sare ya goli tatu kwa tatu

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement