Timu ya Taifa ya wanawake, Twiga stars leo inashuka dimbani kumenyana na timu ya Taifa ya Afrika Kusini, Banyana Banyana katika mchezo wa marudiano kufuzu Mashindano ya Olimpiki 2024, yatakayofanyika Ufaransa.

Katika mchezo huo utakaopigwa saa 2:30 usiku kwenye Uwanja wa Mbombela Afrika Kusini, Twiga inatakiwa kupata ushindi wa mabao manne au zaidi ili ifuzu hatua inayofuata, baada ya awali kuruhusu mabao matatu nyumbani, mchezo uliochezwa Februari 23, 2024, kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi.

Hata hivyo, Twiga itaikosa huduma ya mshambuliaji wake Aisha Masaka ambaye ni majeruhi.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement