Safari ya Twiga Stars kufuzu michuano ya Olimpiki 2024 itakayofanyika Ufaransa imeishia nchini Afrika Kusini katika uwanja wa Mbombela baada ya kupoteza mchezo wa marejeano raundi ya tatu dhidi ya timu ya Taifa ya nchini humo ‘Banyana Banyana’ kwa kufungwa bao 1-0.

Bao pekee la Banyana Banyana walilopata kipindi cha pili cha mchezo huo liliendelea kutengeneza mlima mgumu kwa Twiga kwa kuifanya agrigeti ya 4:0 ambapo twiga stars ilitakiwa kushinda mabao zaidi ya mnne ili kufuzu.


Twiga ilivuka raundi ya tatu baada ya Congo Brazzaville kujitoa kwenye mashindano kisha kuifunga Botswana kwa jumla ya mabao 3-0.

Hata hivyo baada ya ushindi huo Banyana Banyana itacheza mchezo mwingine wa raundi ya 4 ya kufuzu mashindano hayo dhidi ya Nigeria ambao wameitoa Cameroon kwa agrigeti ya 1-0.


You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement