TV3 Tutaonyesha Mechi 170 Za Ligi Ya NBC Championship Msimu Huu
"Ni faraja kwetu kama paytv kufikia hatua hii...Mkataba tunaoenda kusaini leo unaanza mara moja, yaani msimu wa 2023/24 na kupitia Bodi ya Ligi wao wanafahamu zaidi namna. Vilabu vitavyonufaika na mkataba huu".
" Tutaonyesha michezo zaidi ya 170 ya NBC Championship League...tutaonyesha michezo hii kupitia chaneli yetu ya TV3 mnayoifahamu sambamba na Chaneli mpya ya TV3 Sports itayozinduliwa hivi karibuni".
"Msimu huu sisi Tv3, Bodi ya Ligi na TFF tumetazama pamoja mapungufu ya msimu uliopita na tunakwenda kurusha matangazo bora zaidi msimu huu".
"Sisi kama Tv3 tunatambua kuwa hapo awali walikuwepo na wazalishaji maudhui wengine wa Championship na tunatambua walikuwa wanafanya vizuri na sisi tutaingia na kuendeleza pale ambapo waliishi iwe kwenye mapungufu ili mambo yaweze kwenda mbali zaidi".
"Tunaamini tuna uwezo mkubwa kutokana na ukuaji mkubwa ambao tumeufanya tangu kuanzishwa kwetu na tumekuwa tukifanya vizuri hapa nchini na nje ya Tanzania kwa maana ya nchi ambazo Tv3 inaonekana"
Emanuel Sikawa - Mkuu wa vipindi vya Tv3.