TUZO ZA SHIRIKISHO LA SOKA TFF KUFANYIKA KATIKA MECHI YA UFUNGUZI WA MSIMU MPYA WA LIGI KUU
Tuzo za Shirikisho la Soka nchini “TFF” sasa kufanyika wakati wa mchezo wa pazia la ufunguzi wa msimu mpya wa Ligi kwa Maana ya Ngao ya Jamii.
Katika taarifa iliyotolewa na TFF imeeleza kuwa lengo la mabadiliko ya hafla hizo za kuwatuza wachezaji bora wa msimu ni kufanya maboresho ya kulifanya tukio kuwa bora zaidi kukidhi malengo na mahitaji yake.
TFF imeeleza kuwa kwa mabadiliko hayo, hafla ya tuzo za TFF kwa msimu wa 2023/24 itafanyika wakati wa michezo wa Ngao ya Jamii kufungua msimu wa 2024/25.
Ikumbukwe kuwa, Tuzo za TFF ni tukio la kuzawadia wanamichezo waliofanya vizuri katika mashindano yanayoandaliwa na TFF kwa kushirikiana na Bodi ya Ligi kwa maana ya TPLB na matukio mengine rasmi yenye kuambatana na mpira wa Miguu hapa nchini.
Ni hayo tuliyokuwa tumekuandalia kwenye Top Stories kwa siku hii ya leo, kwa updates mbalimbali za kimichezo endelea kufuatilia mitandao yetu ya kijamii………Nikuache na Tagato James Tagato na wachambuzi na kubwa zaidi hii leo tunaangazia juu ya Hafla ya tuzo za msimu wa 2023/24 kufanyika kwenye mechi za Pazia la Ufunguzi wa msimu mpya wa 2024/25.
Lakini hapo baadaye Tutakuwa na Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Almas Kasongo ambapo yeye atatueleza mengi mara baada ya kutamatika kwa Ligi na wamejipangaje katika kuhakikisha msimu ujao unakuwa bora zaidi.