Mchezaji wa Singida Fountain Gate FC, Duke Abuya ameshinda tuzo iliyoambatana na Fedha Shilingi Milioni Moja ya mchezaji Bora kwa mwezi Oktoba ndani ya Klabu ya hiyo.

Abuya ametunukiwa tuzo hiyo baada ya kukidhi vigezo vilivyotumika kumchagua katika mechi zote alizocheza Mwezi Oktoba mwaka huu.

Miongoni mwa vigezo vilivyotumika ni pamoja na nidhamu, msaada wake kwa timu kwenye nafasi anayocheza, Mwendelezo mzuri na kucheza 85% ya mechi zote za Oktoba.

Ndani ya mwezi Oktoba, Singida Fountain Gate amecheza: 

1. Future FC vs Singida FG (CAFCC)

2. Mtibwa Sugar FC vs Singida FG (NBCPL)

3. Singida FG vs Simba SC (NBCPL)

4. Namungo FC vs Singida FG (NBCPL)

5. Yanga SC vs Singida FG (NBCPL)

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement