Tunda akonga nyoyo za mashabiki wa Simba SC
Msanii wa Bongo Fleva Khalid Ramadhani maarufu kama Tunda Man amekonga nyoyo za mashabiki wa klabu ya Simba SC waliojitokeza kwa wingi katika viwanja vya Leaders kwenye hafla ya uzinduzi wa ushirikiano baina ya klabu ya Simba SC na benki ya CRDB unaolenga kutengeza akaunti za mashabiki.