TUNATAKA KUSHINDA KILA TAJI KWA HESHIMA YA JURGEN KLOPP
Beki Conor Bradley anasema Liverpool wanataka "kushinda kila taji" kwa heshima ya kocha anayeondoka Jurgen Klopp baada ya kuichapa Sparta Prague na kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabigwa.
Tayari wakiwa mbele kwa mabao 5-1 baada ya mchezo wa mkondo wa kwanza uliochezwa Jamhuri ya Czech, bao la kwanza la Darwin Nunez lilikuwa la kwanza kati ya mabao manne katika dakika saba za kipindi cha kwanza huku Wekundu hao wakiwalemea wapinzani wao.
Na baada ya mchezo kukamilika wenyeji walikuwa wameshinda kwa jumla ya mabao katika mashindano ya Uropa kwa zaidi ya miongo minne huku wakisawazisha mafanikio ya 11-2 dhidi ya Oulun Palloseura ya Finland katika raundi ya kwanza ya Kombe la Uropa 1980-81.
"Yeye [Klopp] ndiye meneja pekee ambaye nimemfahamu katika klabu hii, kwa hivyo kuondoka kwake kunasikitisha," beki huyo wa Ireland Kaskazini aliambia TNT Sports.
"Tunataka tu kushinda kila kombe tunaloweza kwa heshima yake na kumuaga kwa njia bora zaidi tunayoweza."
Liverpool pia wako katika nafasi ya pili kwenye Ligi ya Premia na watamenyana na Manchester United katika hatua ya nane bora ya Kombe la FA huku wakitarajia kuongeza fedha zaidi kufuatia ushindi wao wa Kombe la Carabao mwezi Februari.