"Tunaamini mwaka huu Wanasimba wameridhika na hata tukipita mtaani tunaona namna wamependeza na jezi zetu. Hongera Sandaland."

"Nafurahi kuwambia baada ya uzinduzi wa jezi hii, jezi zitaanza kupatikana kwenye maduka ya Sandaland. Leo wataanza kupendeza. Nawaomba Wanasimba wanunue na wavae hata wageni wakifika wajue nchi hii ni Simba."

"Tupo African Football League, tumewaacha wengine mbali. Muda ukifika pumba na mchele hujitenga."

"FIFA wameleta mashindano haya kwetu kwa kuangalia namna tunajaza uwanja itakuwa ni aibu uwanja usijae, nawaomba mnunue kwa wingi. Nataka kuona siku hiyo uwanja unatapika."

"Nashukuru serikali inayoongozwa na Rais wetu, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kukubali kufanya marekebisho ya uwanja ule na kutumika kwa ufunguzi wa AFL. Wengine watautumia lakini sababu ya marekebisho ni Mnyama."- Mwenyekiti wa Bodi, Salim Tryagain

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement