Mshambuliaji wa zamani kutokea England Trevor Francis (69), amefariki dunia.

Aliichezea timu ya vijana ya Birmingham City kabla ya kusaini mkataba na Nottingham mwaka 1979 . Uhamisho huo ulihusisha  ada ya pauni 1,150,000 iliyomfanya kuwa nyota wa kwanza wa Uingereza wa pauni milioni 1.

Mwaka 1979 alifunga goli lililoishindia Nottingham kombe lao la kwanza la ubingwa wa Uropa na alikuwemo kwenye kikosi cha klabu hiyo kilichoshinda kombe hilo kwa mara ya pili mwaka 1980.

Amewahi kuchezea klabu mbalimbali ikiwemo Manchester City  pia kushika nafasi za uongozi huko Queens Park Rangers, Sheffield Wednesday,  Birmingham City na Crystal Palace.

Taarifa zinaeleza kuwa Trevor amefariki  kwa mshtuko wa moyo nyumbani kwake Marbella, Hispania.

Klabu ya Nottingham imetuma salamu za rambirambi ikisema kuwa ” Trevor alikuwa mkongwe wa kweli wa Forest ambaye hatasahaulika”.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement