TPLB IMEITOZA LKABU YA SIMBA FAINI KUBWA
Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi ya Bodi ya Ligi Kuu (TPLB) imeitoza klabu ya Simba, faini ya TZS milioni 1 kwa kushindwa kuhudhuria mkutano na wanahabari kuelekea mchezo dhidi ya Yanga SC, Juni 24, 2025.
Huku pia, ikiitoza Simba SC nyingine ya TZS milioni 1 kwa kushindwa kuhudhuria kikao cha kitaalamu cha maandalizi ya mchezo huo.
Kamati hiyo maarufi kama Kamati ya saa 72, pia imeichapa faini nyingine klabu hiyo ya TZS milioni 1 kwa kuingia uwanjani wakitumia mlago usio rasmi katika siku ya mchezo huo.



