Timu za wanawake za Simba na Yanga zitashuka dimbani leo saa 10:00 jioni kucheza mchezo wa Ligi Kuu (WPL) mchezo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Huu ni mchezo wa pili kwao kukutana kwenye msimu huu wa ligi 2023/2024, huku mara ya kwanza Yanga Princess ilipoteza kwa mabao 3-1.

Kwenye msimamo wa Ligi hiyo Simba Queens ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 31 ikicheza mechi 11, huku Yanga Princess ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 21 ikicheza mechi 10.

Yanga Princess imeingia uwanjani kupitia mlango wa mashabiki ikiwa ni muda chache kabla ya kuanza kwa mtanange wa Ligi Kuu ya wanawake kati yao na Simba Queens.

Saa 10:00 jioni timu hizo mbili zitakutana kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi katika mwendelezo wa WPL ambayo mzunguko wa kwanza Yanga ilipokea kichapo cha 3-0.

Wakati timu hizo zinatoka vyumbani na kuingia uwanjani Yanga iliingia kwa kutumia geti wanalopita mashabiki huku Simba ikiingia eneo sahihi.

Timu hizo mbili zinanolewa na makocha wasaidizi ambao walikuwa manahodha wa zamani wa timu za wanaume, kwa Simba ambaye ni Mussa Hassan 'Mgosi' na Fredy Mbuna ambaye anaifundisha Yanga.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement