TIMU YA WANAWAKE YA SIMBA LEO KUTANGAZA UBINGWA ENDAPO AKISHINDA
Timu ya wanawake ya simba maarufu kama Simba queens leo inanafasi kubwa ya kua MABINGWA wapya endapo kama watashinda mchezo wa leo
Timu ya Alliance girls leo watakua uwanjani wakiwaalika Simba queens katika muendelezo wa ligi hii ya wanawake kurejea baada ya muda mfupi sasa leo kama atashinda atakua bingwa
Kumbuka msimu ulio pita TIMU ya JKT queens walikua mabingwa lakini msimu huu Simba wapo siriasi kuchukua ubingwa maana leo ni mchezo wa 16 wanaenda kucheza lakini michezo kumitano hawajafungwa mechi hata moja
Msimamo unaonesha kuwa Simba queens points 43 LAKINI JKT queens points 34 hivyo endapo akipata alama 3 kutakua hakuna klabu ambayo itaweze kufikia alama hizo Lakini mbali na hilo upande wa binti Aisha Mnunka akiwa na mabao 18 mbele ya Stumai Abdallah hivyo Simba queens wananafasi kubwa kurejesha UTAWALA wao
Endapo AKISHINDA leo basi atakata ticket ya moja kwa moja kwenda kushiriki michuano ya KLABU bingwa barani Africa