Ujerumani imeandika rekodi ya kuwa timu ya kwanza kutinga hatua ya 16 bora Euro 2024 baada ya kuifunga Hungary mabao 2-0 katika uwanja wa MHP Arena nchini Ujerumani.

Mabao ya Jamal Musiala na Ikay Gundogan yametosha kuipa Ujerumani ushindi huo na kufikisha pointi sita katika msimamo wa kundi A.

Gundogan ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mchezo huo akifunga na kutoa pasi ya bao la kwanza.

Kundi hilo lenye vinara Ujerumani, Switzerland nafasi ya pili na pointi 3 huku Scotland na Hungary zikiwa hazina pointi hata moja.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement