TIMU YA TAIFA YA HISPANIA YAINGIA FAINALI KATIKA MASHINDANO YA EURO 2024 KWA KUIFUNGA UFARANSA 2-1
Lamine Yamal amekuwa mfungaji mwenye umri mdogo zaidi katika historia ya michuano ya Uropa wakati Uhispania ilipoilaza Ufaransa katika shindano la kutinga fainali ya Euro 2024.
Baada ya Randal Kolo Muani kufunga bao kwa kichwa kutoka kwa pasi ya Kylian Mbappe na kuwapa Ufaransa bao la mapema, Yamal alifunga bao lake la kwanza kutoka nje ya eneo la hatari na kuandika jina lake kwenye vitabu vya rekodi kwa kufunga akiwa na umri wa miaka 16 na siku 362.
Bao la Yamal lilipatikana dakika ya 21, na Uhispania walikuwa mbele dakika nne baadaye huku shambulio la Dani Olmo likimgusa beki wa Ufaransa, Jules Kounde na kuingia wavuni.
Ufaransa ilibidi wajitokeze kupambamba zaidi baada ya kipindi cha kwanza cha kusisimua na walifanya hivyo, huku Aurelien Tchouameni akiokoa mpira wa kichwa na Mbappe akinyimwa nafasi licha ya juhudi zake kubwa za kutafuta bao la kusawazisha.
Nahodha huyo wa Ufaransa, akicheza bila barakoa jeusi kwa mara ya kwanza tangu avunjike pua mwanzoni mwa michuano hiyo, alipata nafasi kubwa ya kusawazisha dakika za mwisho - lakini alifanya shambulizi lililopaa juu ya lango.
Uhispania ilifanya mashambulizi mengi zaidi kwenye mechi hiyo huku Ufaransa, kwa upande wao, walifanya mashambulizi machache dhidi ya timu ambayo itamenyana na England au Uholanzi katika fainali ya Jumapili.