TIMU TANO ZAWEKWA KIZUIZINI KUSAJILI WACHEZAJI WAPYA KUTOKANA NA MADENI
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) pamoja na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imezifungia klabu zifuatazo kusajili mpaka zitakapowalipa wachezaji wanaozidai;
1. Young Africans
2. Singida Fountain Gate FC
3. Tabora United FC
4. Biashara United FC
5. FGA Talents FC
Klabu ambayo itawalipa wahusika, itaondolewa mara moja adhabu ya kufungiwa kusajili. Hadi leo asubuhi kupitia mfumo wa FIFA (FIFA legal portal) hakuna taarifa ya klabu yoyote kati ya hizo iliyowalipa wahusika.