TIMU 12 KUTOKA MATAIFA TOFAUTI KUKUTANA KATIKA MICHUANO YA CECAFA DAR PORT KAGAME CUP INATARAJIWA KUANZA JIJINI DAR ES SALAAM
Michuano ya CECAFA Dar Port Kagame Cup kuanza kutimua vumbi hapo kesho mpaka Julai 21 jijini Dar es salaam kwa timu 12 kutoka mataifa tofauti ya Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati kumenyana ambapo mbali na wageni Red Arrows FC ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu ya Zambia, timu nyingine zote zinatoka ndani ya Ukanda huo.
Timu za Ligi Kuu ya Tanzania Bara Simba Sports Club na AFC Leopards kutoka Kenya zimeshinda taji la ukanda huo mara sita, Young Africans SC, Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara na Tusker FC ya Kenya pia wametwaa Kombe hilo mara tano kila mmoja.
Lakini kutokana na kukosekana kwa klabu nne katika Kombe la Kagame la Dar Port Kagame 2024, APR FC (Rwanda), Gor Mahia (Kenya) na Sports Club Villa ya Uganda zitakuwa timu tatu zenye shauku ya kushinda Kombe la Kagame kwa mara ya nne.
Ingawa Gor Mahia FC walinyanyua kombe hilo mara ya mwisho mwaka wa 1985 walipowashinda mahasimu wao AFC Leopards mabao 2-0 kwenye fainali, sasa wana timu inayoonekana kuwa imara ambayo ina uwezo wa kusonga mbele ambapo hivi karibuni iliwasajili kocha wa Brazil Leonardo Martins Neiva na wachezaji wapya Samuel Kapen, Chris Pius Akena, na Gideon Bendeka.
Kwa APR FC ambao wametawala Soka la Rwanda kwa miaka kadhaa, watakuwa na njaa zaidi ya kuthibitisha kwamba wana kile kinachohitajika chini ya kocha mpya Darko Novic.
Kwa SC Villa ambao walitwaa tena taji la Ligi Kuu ya Uganda baada ya miaka 20.
Azam FC kutoka Tanzania ambao wametwaa Kombe hilo mara mbili pia hawatashiriki Michuano hiyo kama ilivyo kwa Simba SC na Yanga SC.
Michuano hiyo ambayo itafanyika katika Dimba la Chamazi na KMC - Kundi A Coast Union FC (Tanzania), Al Wadi FC (Sudan), JKU SC (Zanzibar), Dekedaha FC (Somalia)
Kundi B: Al Hilal (Sudan), Gor Mahia FC (Kenya), Red Arrows FC (Zambia), Djibouti Telecom (Djibouti)
Kundi C: SC Villa (Uganda), APR FC (Rwanda), Singida Black Stars (Tanzania), El Merriekh Bentiu (Sudan Kusini)