TIMOTHY THOBIAS ATASALIA NJE YA UWANJA KWA MIEZI 6 NA FAINI YA SH. 500,000 HUKU OMARY NASSORO AKIFUNGIWA MECHI 12
Adhabu hii ni kwa kuzingatia Kanuni ya 17:60 ya Ligi ya Championshipkuhusu Taratibu za Mchezo.
Mchezaji Timothy Thobias Timothy wa timu ya TMA amefungiwa michezosita (6) na kutozwa faini ya Sh. 500,000 (laki tano) kwa kosa lakumtukana mwamuzi wa mchezo tajwa hapo juu wakati timu zikiendamapumziko.
Adhabu hii ni kwa kuzingatia Kanuni ya 41:5(5.3) ya Ligi ya Championshipkuhusu Udhibiti kwa Wachezaji.
Mchezaji Omary Nassoro Matwiko wa timu ya TMA amefungiwa michezo 12 na kutozwa faini ya Sh. 500,000 (laki tano) kwa kosa la kumtukanamwamuzi wakati timu zikienda mapumziko katika mchezo tajwa hapona kuwaongoza mashabiki waliovamia eneo la kuchezea kumshambuliamwamuzi huyo na kumpiga ngumi kwenye paji la uso.
Baada ya mchezo kumalizika, mchezaji huyo (Omary Nassoro Matwiko)ambaye alikuwa ameshaonyeshwa kadi nyekundu aliendeleakumshambulia mwamuzi na kutaka kumpokonya simu yake kabla yakudhibitiwa na askari polisi.
Adhabu hii ni kwa kuzingatia Kanuni ya 41:5(5.3) ya Ligi ya Championship kuhusu Udhibiti kwa Wachezaji.
Kutokana na kukithiri kwa matukio ya kiuamuzi yaliyozua utata katika mchezo huo, Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi imewapeleka waamuzi wa mchezo tajwa hapo juu kwenye Kamati ya WaamuzĂ kwaajili ya kufanyiwa tathmini ya kiwango chao cha kutafsiri sheria 17 za mpira wa miguu katika mchezo huo.