TIGER WOODS AACHANA NA NIKE BAADA YA MIAKA 27
mchezaji maarufu wa gofu Tiger Woods ametangaza kuachana na mdhamini wake wa muda mrefu NIKE baada ya kudumu naye kwa miaka 27
Woods, ambaye amekuwa akishitikiana na chapa maarufu ya michezo tangu 1996, alitoa tangazo hilo kwenye mitandao ya kijamii, na kuwaacha mashabiki na wapenzi wa tasnia wakiwa na mshangao
Woods alitoa taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram .alisema” Zaidi ya miaka 27 iliyopita, nilibahatika kuanzisha ushirikiano na moja ya chapa maarufu zaidi ulimwenguni," Woods alisema. "Siku nilizokuwa nao zimejazwa na matukio na kumbukumbu nyingi za kushangaza, ikiwa ningeanza kuzitaja, ningeweza kuzitaja bila kumaliza, Shauku na maono ya Phil Knight yalileta ushirikiano huu wa Nike na Golf ningependa kumshukuru yeye binafsi, pamoja na wafanyakazi wa Nike na wanamichezo wote ambao nimekuwa na furaha ya kufanya kazi nao”