Kocha wa Bayern Munich Thomas Tuchel ameweka wazi kuwa anajiona kuwa na wakati mgumu zaidi katika mchezo wa Mkondo wa pili Nusu Fainali Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya mara baada ya kutoka sare ya bao 2-2 dhidi ya wapinzani wao Real Madrid.

Tuchel ameeleza kuwa amesikitishwa na kikosi chake baada ya kukosa nafasi ambazo zingewapatia ushindi wa bao 3 katika mchezo huo ambao kwa upande wao ungekuwa na faida kubwa katika Uwanja wa nyumbani.

Tuchel aliendelea kusisitiza umuhimu wa kushinda huko Madrid, na baadaye kuakisi kile alichosema kabla ya mechi ya mkondo wa kwanza, na hivyo kuuita mchezo wa 50-50.

Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya inaendelea kutimua vumbi hii leo kwa mchezo mwingine wa Nusu Fainali, Dortmund dhidi ya PSG.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement