Mshambuliaji wa klabu ya Bayern Munich na timu ya taifa Ujerumani, Thomas Muller ametangaza kustaafu soka la kimataifa akiwa na umri wa miaka 34 ikiwa ni siku moja baada ya kutamatika kwa mashindano ya kombe la Mataifa Ulaya EURO 2024 iliyofanyika Nchini Ujerumani.

Muller ambaye ni mshindi wa kombe la Dunia 2014 ameifungia Ujerumani magoli 45 na kusaidia mengine 41 kwenye mechi 131. Muller alikuwa mfungaji bora kwenye michuano ya kombe la Dunia 2010 iliyofanyika Nchini Afrika Kusini.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement