Aliyekuwa kiungo wa Barcelona, Bayern Munich, Liverpool na Timu ya taifa ya Uhispania, Thiago Alcantara ameamua kustaafu soka la kulipwa akiwa na umri wa miaka 33.

Thiago ambaye mkataba wake na Liverpool ulitamatika mwishoni mwa msimu uliopita alianza maisha yake ya soka kwenye shule ya kukuza vipaji ya Barcelona almaarufu La Masia na kupandishwa kwenye timu ya wakubwa mnamo Julai 1, 2011.

Mnamo Julai 14, 2013 alijiunga na Bayern Munich ya Ujerumani na kudumu kwa miaka 7 kabla ya kutimkia Liverpool mnamo Septemba 18, 2020.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement