MTENDAJI Mkuu wa Tabora United, Thabit Kandoro amejiuzulu nafasi hiyo siku chache baada ya kumtimua aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Goran Kopunovic.

Kandoro amejiengua nafasi hiyo kutokana na kukabiliwa na matatizo ya kifamilia.

Wakati baadhi ya viongozi waking'oka, inasemekana makocha wawili, Denis Goavec, kocha mkuu na Masoud Djuma, waliotua kuchukua nafasi ya Goran bado hawajamalizana na uongozi wa timu hiyo.

"Ni kweli Kandoro kajiweka pembeni kutokana na matatizo yake binafsi na tayari kawasilisha barua ya kujiweka pembeni, kinachosubiriwa ni majibu kutoka kwa viongozi," amesema.

Kuhusu kocha mkuu, chanzo hicho kilisema ni kweli kocha hajasaini mkataba lakini ni suala la muda kwani kilichobaki ni kufanya hivyo tu kwasababu mazungumzo baina yao yamekamilika.

Alipotafutwa Ofisa Habari wa Tabora United, Christina Mwagala amesema "Sitaki kuzungumza mambo mengi, kama suala hilo lipo mtaona taarifa kutoka ndani ya uongozi tusubiri muda ukifika watafanya hivyo."

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement