Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeufungulia uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora kutumika kwa michezo ya Ligi baada kufanya marekebisho yaliyokidhi vigezo vya kikanuni na sheria za mpira wa miguu.

Uwanja huo uliofungiwa kutokana na eneo la kuchezea (pitch) kutofaa kuchezewa mpira kama ilivyoainishwa kwenye masharti ya Kanuni ya Leseni za Klabu umekaguliwa na kukidhi vigezo vya Kikanuni baada ya marekebisho yaliyoelekezwa kufanyika.

Tabora United ambayo inatumia uwanjani huo kwa michezo yake ya nyumbani sasa inaweza kuutumia uwanja huo.

TFF inaendelea kuzikumbusha klabu za Ligi Kuu ya NBC, Ligi ya NBC ya Championship na First League kuendelea kuboresha na kutunza miundombinu ya viwanja vyao vya nyumbani kwa kushirikiana na wamiliki (kwa klabu ambazo hazimiliki viwanja), ili michezo ya Ligi ichezwe kwenye viwanja bora vinavyosaidia kuongeza ushindani na thamani ya Ligi.

Taarifa hiyo imetolewa na ofisa habari na mawasiliano TFF Cliford Mario Ndimbo leo hii.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement