Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limemfungia mechi nane kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Adel Amrouche, hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF.

Adhabu hiyo iliyotolewa na Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho hilo la Mpira, inafuatia malalamiko yaliyowasilishwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Morocco dhidi ya kocha huyo.

Malalamiko hayo yametokana na kauli tata alizozitoa Amrouche kwa kudai kuwa, Timu ya Morocco ina ushawishi ndani ya CAF, imesema taarifa hiyo.

Katika taarifa hiyo hiyo, TFF imesema imemsimamisha Kocha Adel Amrouche.

Hemed Morocco akisaidiwa na Juma Mgunda watashikilia nafasi ya Amrouche huku Taifa stars ikisalia na mechi moja katika hatua ya makundi katika Dimba la AFCON2023.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement