Katika kuhakikisha hadhi ya Ligi kuu ya Zanzibar inakuwa, Serikali imeweka mipango mikakati ya kuhakikisha Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Shirikisho la Soka Zanzibar (ZFF) wanashirikiana katika mambo mbalimbali ya kisoka.

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma amesema Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF) wanashirikiana katika mambo mbalimbali yanayohusu soka kubwa likiwa ni katika uteuzi wa wachezaji wanaounda Timu za Taifa.

Naibu Waziri Mwinjuma amesema hayo hii leo Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu Swali la Mwanakhamisi Kassim Said wa Jimbo la Magomeni aliyeuliza, TFF inashirikianaje na ZFF kupandisha hadhi Ligi ya Zanzibar.

"TFF imekua ikishirikiana na ZFF katika uteuzi wa wachezaji kwa Timu za Taifa za vijana, ambapo vijana kutoka Zanzibar wamekuwa wakiitwa katika timu hizo na hatimaye kucheza Timu ya Taifa ya wakubwa" amesema Naibu Waziri Mwinjuma.

Naibu Waziri Mwinjuma amesema Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania chini ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imekua ikishirikiana na ZFF katika Mipango mbalimbali na kubainisha kuwa hivi karibuni kutakua na Mafunzo ya uendeshaji wa Bodi ya Ligi ya Zanzibar ambayo itajikita katika Menejimenti, uwekezaji, Udhamini na Masoko ili kuendeleza soka katika pande mbili za Muungano.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement