Mwanasoka wa kike, Temwa Chawinga (25) amewashinda Cristiano Ronaldo, Harry Kane na Kylian Mbappe na kuwaongoza kwenye orodha ya ufungaji mabao duniani mwaka 2023.

Mwanadada huyo raia wa Malawi alifunga mabao 63 katika mashindano ya Ligi Kuu ya Wanawake huko China akiwa na kikosi cha Wuhan Jianghan University FC akimzidi Cristiano Ronaldo mabao 9 huku akifunga jumla ya mabao 83 katika jumla ya mechi 84 za mashindano yote aliyashiriki akiwa na Jianghan.

Chawinga ni mchezaji wa tatu mfululizo wa wanawake kushinda tuzo hiyo baada ya Mhispania Jenni Hermoso kuongoza msimamo mwaka wa 2021 na Fenna Kalma wa Uholanzi mwaka 2022.

Ronaldo alimaliza msimu wa 2023 akiwa na mabao 54 kwa mwaka huo huku Kane na Mbappe wakiwa na jumla ya mabao 52.

Kwasasa mwanadada huyo analisakata kabumbu akiwa ndani ya Kansas City Current huko America.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement