Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Qatar nchini Tanzania Fahad Rashid Al Marekhi kuhusu ushirikiano katika sekta za Utamaduni, Sanaa na michezo.

Katika kikao hicho viongozi hao pamoja na mambo mengine wamekubaliana kukamilisha taratibu za utiaji saini wa Hati za makubaliano (MoU) ili utekelezaji wa maeneo hayo ya ushirikiano katika sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo uanze kufanyika baina ya nchi hizo.

Kikao hicho kimehudhuriwa pia Naibu Katibu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Suleiman Serera, Wakurugenzi wa Idara na Vitengo vya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Mhe. Balozi Abdalah A. Kilima.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement