Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Gerson Msigwa amekutana na kufanya mazungumzo na Mshindi wa Miss Planet International na Miss Natural Beauty 2022 Eva Paul kuhusu namna watakavyoshirikiana kufanikisha Tamasha la Tanzanite ambalo linatarajiwa kufanyika mapema 2024 nchini.

Katibu Mkuu Bw. Msigwa amesema hayo Desemba 06, 2023 alipofanya mazungumzo na mshindi huyo ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma.

“Nampongeza Eva Paul kwa ubunifu huu mkubwa alioufanya, yeye ameamua kufanya tamasha hili akijielekeza kutangaza madini ya aina ya tanzanite yanayopatikana Tanzania, tumejadiliana kulifanya tamasha hili kuwa kubwa na nimeelekeza Idara ya Sanaa wafanye kazi pamoja ya kuangalia fursa zilizopo ili kulifanya tamasha hili kuwa kubwa” amesema Katibu Mkuu Bw. Msigwa.

Katibu Mkuu Bw. Msigwa amesema kuwa matamasha kama hayo ndiyo yanaitangaza nchi na kuleta faida za kiuchumi kwa kuwa unap[otangaza madini ya Tanzania uanatangaza pato la taifa.

Ameongeza kuwa ili kufanikisha tamasha hilo, wizara yake itashirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Wizara ya Madini hatua ambayo itawakusanya warembo kutoka nchi mbalimbali duniani kwa kuwa Tanzania ina vivutio vingi nchi nzima.

Kwa upande wake mshindi huyo na mwandaaji wa tamasha la Tanzanite Eva Paul amesema kuwa amechagua kuyatangaza madini ya tanzanite ili kumuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kutangaza utalii wa madini duniani kote kwa kuwa Tanzania ni nchi pekee yenye madini ya tanzanite.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement