WAKATI wachezaji watatu wa Yanga, Ibrahim Hamad ‘Bacca’, Mudathir Yahya na Clement Mzize wakirejea kikosini baada ya majukumu ya timu ya taifa ‘Taifa Stars’ wengine wanne wanatarajiwa kuingia nchini leo.

Takriban wachezaji tisa wa kikosi cha kwanza cha Yanga walikuwa kwenye majukumu ya timu za taifa ambazo zilicheza mechi za michuano ya kirafiki ya FIFA Series.

Habari kutoka chanzo cha ndani ya Yanga kimesema nyota wanne, Pacome Zouzoua (Ivory Coast), Stephane Aziz KI (Burkina Faso), Kennedy Musonda (Zambia) na Djigui Diara (Mali) wanatajiwa kuingia nchini Jumatano kujiunga na wenzao kwa ajili ya mechi na Mamelodi.

Yanga itashuka kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jumamosi hii (Machi 30) kucheza mechi ya mkondo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundownds kuanzia saa 3 kamili usiku.

“Tumewasiliana na mataifa yao na wametukubalia hivyo wengine wanne wa kimataifa watajiunga na wenzao kambini Jumatano Machi 27 kuiwahi mechi ya Mamelodi itakayochezwa Jumamosi,” kilisema chanzo hicho.

Wakati Yanga wakifurahi juu ya urejeo wa nyota wao muhimu, kwa Simba wachezaji Kibu Denis ambaye tayari yuko nchini na Saido Ntibazonkiza anatarajia kurudi kutoka Burundi Jumatano kuiwahi mechi ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri Kwa Mkapa Ijumaa hii.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement