Klabu ya tabora united imepotea nyumbani mbele ya JKT Tanzania katika mchezo wa mtoano wa kuwania kubaki ligi kuu, Katika mchezo huo tabora united ilifungwa magoli 4 kwa 0 Katika kiwanja cha Ali Hassan Mwinyi.

Katika Mchezo huo mkuu wa mkoa wa Tabora alitoa ahadi hiyo kwa lengo la kuongeza hamasa na motisha ili waweze kujikwamua lakini bado mambo yakawa magumu mbele ya maafande

Lakini kumekua na malalamiko kutoka tabora united wakidai kukandamizwa na maamuzi ya waamuzi YAANI Sheria namba 5 imevunja Sheria namba 11 kwa maana goli la kwanza na goli la pili yalipaswa kua ni offside kwa maan mchezaji wa JKT Tanzania alikua katika eneo la kupoteza

Kufuatia matokeo hayo sasa TABORA UNITED inapaswa kushinda magoli ma 5 ili waweze kujinusuru kutocheza Mchezo mwingine wa mtoano dhidi ya Biashara utd ambao wa wanasubiri Mshindwa wa jumla Katika Mchezo huo

Kumbuka timu hizi 2 JKT Tanzania na Tabora united wote walipanda ligi kuu MSIMU ulio pita kutokea NBC championship league na sasa TABORA UNITED wanaonekana kutokua na matumaini ya kusalia licha ya kwamba wananafasi ya kucheza mchezo mwingine

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement