TABORA UNITED YAACHANA NA KOCHA WAKE GORAN COPUNOVIC YAMPA MKATABA KOCHA MPYA MFARANSA
TIMU ya Tabora United imeachana na kocha wake Goran Copunovic baada mfululizo wa matokeo mabaya kwenye Ligi kuu ya Tanzania bara. Tayari Tabora United wametangaza kocha mpya kutoka Ufaransa, Denis Laurent Goevec ambaye amesaini mkataba wa mwaka mmoja Goavec amewahi kuvinoa vikosi vya AS Vita Club ya DR Congo na JS Saoura ya Algeria.
Katika mechi 21 ilizocheza kwenye Ligi Kuu, Chini ya kocha Gorani Kopunovic timu ya Tabora United imepata ushindi mara nne tu, ikitoka sare tisa na kupoteza michezo saba.