Klabu ya Tabora United imefungiwa kusajili mpaka itakapowalipa wachezaji Emanuel Lamptey pamoja na Collins Gyamfi 

Uamuzi huo umefanywa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu baada ya wachezaji Emanuel Lamptey pamoja na Collins Gyamfi kufanikiwa kushinda kesi ya madai dhidi ya klabu hiyo. 

Wachezaji hao raia wa Ghana walifungua kesi FIFA wakidai malipo ya ada ya Usajili na malimbikizo ya mishahara. 

Klabu hiyo ilitakiwa iwe imewalipa ndani ya siku 45 tangu uamuzi huo ulipotolewa lakini hawakutekeleza hukumu hiyo. 

Wakati FIFA imefungia klabu hiyo kufanya uhamisho kwa wachezaji wa kimataifa Shirikisho la Soka la Tanzania "TFF" limezuia timu hiyo kufanya uhamisho wa ndani. 

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement