Tanzania Prisons, Tabora United leo zimeshindwa kufurukuta nyumbani baada ya kubanwa na kutoka sare ya 1-1 kwenye mchezo wa raundi ya 17.

Tabora imetoka sare dhidi ya Singida Fountain Gate katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mbele ya Singida Fountain Gate na Prisons ikilazimisha sare dhidi ya Azam FC, Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Singida ilitangulia kuapata bao kutoka kwa beki wake Yahya Mbegu dakika ya 53 na Tabora ililazimika kusubiri dakika saba kabla ya pambano hilo kumalizika na kuchomoa bao lililowekwa kimiani kwa kichwa na Mganda John Ben Nakibinge.

Tanzania Prisons walipata bao mapema kupitia kwa straika, Samson Mbangula na Azam FC kusawazisha kwa mkwaju wa penalti baada ya beki na Nahodha wa Prisons Jumanne Elfadhir kuunawa mpira eneo la hatari na mwamuzi Ally Mnyupe (Morogoro) kuamuru adhabu hiyo.

Mchezo ujao Maafande hao wanabaki Sokoine kuwakaribisha Tabora United huku Azam wakiwafuata Singida FG.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement