Raia wa Malawi na mshambuliaji wa klabu ya Paris Saint-Germain, Tabitha Chawinga ametunukiwa tuzo ya mchezaji bora kwenye ligi ya soka ya wanawake Ufaransa kwa msimu wa 2023/24.

Tabitha, mwenye umri wa miaka 27, amezoa tuzo hiyo katika msimu wake wa kwanza ligi ya Ufaransa, huku pia akielekea kushinda kiatu cha dhahabu, kwenye ligi hiyo baada ya kufunga mabao 18.


Msimu uliopita, wakati akichezea klabu ya Italia ya Inter Milan, Tabitha alutunukiwa tuzo ya mfungaji bora baada ya kufunga magoli 23 katika mechi 21.

Pia ni Mmalawi wa kwanza kufunga bao katika mashindano ya Kombe la Mabingwa bara Ulaya kwa upande wa wanawake.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement