SVEN-GORAN ERIKSSON ABAKIZA SIKU CHACHE ZA KUISHI
Kocha wa zamani wa England Sven-Goran Eriksson amefichua kuwa amegundulika kuwa na saratani na amebakiza mwaka moja wa kuishi
Eriksson mwenye umri wa miaka 75 amesema yupo kwenye kipindi amabacho anajitahidi kuishi vizuri kadri awezavyo kwani siku zake za kukaa duniani zinahesabika japo madaktari hawawezi kusema siku halisi lakini inakadiriwa ni miezi 12 hata hivyo madaktari wana jitahidi kadri ya uwezo wao kupamabana na swala Hilo.
Eriksson, ambaye aliiongoza Uingereza kwa miaka mitano kabla ya kuondoka baada ya Kombe la Dunia la 2006, alijiuzulu nafasi yake ya hivi majuzi kama mkurugenzi wa michezo katika klabu ya Karlstad ya Uswiswi miezi 11 iliyopita kutokana na matatizo ya kiafya.