Klabu ya stand United ambayo makazi yake ni kule shinyanga imaanza kusuka mipango mapema ikiwa bado takribani miezi 3 kuanza kwa msimu mpya wa NBC championship league 2024/2025.

Kuelekea msimu huo timu ya stand United imeanza vikao vyake kupitia mkuu wa wilaya mh.Julius Mtatilo kwajili ya kufanya maandalizi,Vikao hivyo vinavyo endelea lengo ni kuona sapoti ya wadau na baadhi ya viongozi kama vile mkuu wa mkoa na wabunge wapale shinyanga kutoa sapoti.

Hata hivyo inaonesha kua Serikali ya mkoa wa shinyanga imeonesha nia ya dhatii kabisa kutoa sapoti, swali imekua je wanataka kuivuta timu hii kua chini ya harmashauri au itakua ni msaada tu.

Kumbuka stand United ilipanda daraja msimu jana kutokea First league division nakua bingwa wakaja NBC championship league wakafanikiwa kubaki baada ya kucheza playoff na kuwaondoa COPCO FC.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement