Singida Fountain Gate, imesonga mbele katika hatua ya 16 bora michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), baada ya kuifunga FGA Talents mabao 2-0.

Timu hiyo imepata ushindi huo leo Februari 19, 2024 mbele ya FGA Talents ya mkoani Morogoro, inayoshiriki Ligi ya Championship, katika Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza katika mchezo wa raundi ya tatu (32 bora), ambao umeanza saa 10:00 jioni.

Singida ambayo imehamishia mechi zake za nyumbani Uwanja wa CCM Kirumba, imepata mabao yake kupitia kwa Mkongomani, Francy Kazadi dakika ya 11 akimalizia vyema pasi ya Dickson Ambundo.

Matajiri hao wa alizeti walienda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 2-0 baada ya Dickson Ambundo, kuifungia bao la pili dakika ya 45 kwa mkwaju mkali akiwatambuka mabeki wa FGA Talents.

Dakika ya 88, FGA Talents wamekosa nafasi muhimu ya kusawazisha bao, baada ya mshambuliaji wa timu hiyo, Zamfuko Elias, kukosa mkwaju wa penalti.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement