Singida Fountain Gate FC imetangaza kuvunja benchi la ufundi lote liliokuwa linaongozwa na Kocha Mkuu Thabo Senong kisa matokeo mabovu ya timu hiyo.

Taarifa hiyo imetolewa na Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo inasema "Bodi na Menejimenti ya Singida Fountain Gate FC imefikia uamuzi wa kuvunja benchi lote la ufundi lililokuwa likiongozwa na Kocha Thabo Senong kufuatia mfululizo wa matokeo mabaya ya timu hiyo."

"Kufuatia uamuzi huo, uongozi utatangaza benchi jipya la ufundi muda wowote kutoka sasa" ilimaliza taarifa hiyo.

Singida imecheza mechi nane za Ligi bila ushindi tangu ilipoifunga Coastal Union mabao 2-1 Novemba 27, 2023 katika Uwanja wa Liti, Singida.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement