Miguel Gamondi kocha wa Yanga amesema katika makipa watano bora kwenye Afcon ya msimu huu, Diarra yumo.

Diarra alicheza mechi zote za Afcon katika timu yake ya Taifa ya Mali,mpaka walipotolewa hatua ya robo fainali dhidi ya Ivory Coast dakika za mwishoni.

Anaporejea katika kikosi chake cha Yanga Alhamisi hii, kocha wake Gamondi amempongeza pia Aziz KI kwa kiwango kizuri ingawa hajafunga bao lolote ila hakuwasahau wachezaji wa Taifa Stars amesema walifanya kazi nzuri.

"Ndani ya kikosi changu Diarra ni shujaa kwa hatua ambayo amefika na Taifa lake la Mali nina amini mashabiki wa timu hiyo watampokea kwa heshima.

"Wachezaji sasa wanarejea klabuni kwao wanatakiwa kusahau kuhusu matokeo ya Afcon na badala yake waendeleze makali yao na kama wamelikosa taji la Afcon basi watapata wakiwa na Yanga," amesema Gamondi.

Diarra katika michuano hiyo amecheza dakika 450.

Katika mechi hizo ameruhusu jumla ya mabao manne huku timu yao ikiwa imefunga jumla ya mabao 6 katika michezo mitano.

Chanzo kimoja Kiliandika kuwa simu zimeanza kuita kwa kipa huyo kutokana na uwezo mzuri aliouonyesha, hivyo huenda baada ya msimu huu Yanga watakuwa na kibarua kigumu kuweza kushindana na vigogo kumbakiza mchezaji huyo.

Diarra, kipa namba moja wa Yanga, alifanya kazi kubwa msimu uliopita nakuifikisha timu hiyo kwenye fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement