Mkurugenzi wa Sheria wa Klabu ya Yanga, Simon Patrick amesema Klabu ilipata taarifa kuna kundi la watu limepeleka maombi Mahakamani kuomba uongozi wa Yanga uondolewe na wakabidhiwe klabu wakitumia Sahihi za Kughushi.


Simon amefafanua zaidi akisema “Tuligundua Juma Ally Abeid (Magoma) aligushi sahihi na kujifanya Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini, aligushi sahihi ya Mama Fatma Karume, aligushi sahihi la Mzee Jabil Katundu ambaye alilazimishwa kuingia kwenye hili shauri.”

Pia, ameongeza Wamegundua kuna Watu nyuma ya walalamikaji wanatumika kusababisha Vurugu na hivyo Klabu inashirikiana na Vyombo vya Usalama kuchunguza walionyuma ya mpango huo.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement