Klabu ya ligi Kuu ya NBC YA Simba imefungiwa kusajili mpaka itakapolipa madai ya Klabu ya Teungueth ya Senegal kuhusu mchezaji Pape Ousmane Sakho.

Uamuzi huo umefanywa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (TFF) baada ya klabu hiyo kushinda kesi ya madai dhidi ya Simba kutokana na mauzo ya Sakho. Kabla ya kujiunga na Simba, Sakho ambaye hivi sasa anacheza timu ya Quevilly Reuen Metropole ya Ufaransa alikuwa mchezaji wa Simba.

Klabu hiyo ilifungua kesi FIFA dhidi ya Simba ikidai sehemu ya malipo kutokana na mauzo ya Sakho. Simba ilitakiwa iwe imetelekeza uamuzi huo ndani ya siku 45 tangu ulipotolewa, lakini haikufanyika hivyo.

Wakati FIFA imeifungia klabu hiyo kufanya uhamisho wa wachezaji kimataifa, TTF limeifungia Simba kufanya uhamisho wa ndani.

TTF inazikumbusha klabu kuheshimu sheria, kanuni na taratibu za mpira wa miguu ili kuepusha adhabu mbalimbali, ikiwemo kufungiwa usajili wachezaji

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement