1. TUTAENDELEZA UBABE KWA YANGA WIKI HII

"Mkutano wetu unahusu maandalizi kuelekea mchezo wa wiki hii dhidi ya watani zetu wakubwa, Young Africans SC."

"Mchezo dhidi ya Yanga SC utachezwa siku ya Jumapili Novemba 5, 2023 saa 11:00 jioni katika Uwanja wa Mkapa. Ni mechi kubwa kwetu, ni mechi ambayo inakwenda kuonyesha ubora halisi ya mpira wa Tanzania na ushindi wake unaleta tabasamu kwa mashabiki wa timu husika na kupoteza kunaacha majonzi."

"Ni mechi ambayo tunakwenda kuendeleza ubabe kwa watani zetu. Ili tujiridhishe kwamba msimu huu tutafanya vizuri ni kupata ushindi katika mchezo huo. Tunataka tuchukue ubingwa mapema sana, katika hili tunawashukuru Ihefu kwa kutusaidia kazi na sisi tunataka kuendeleza kuweka tofauti ya alama na Yanga SC."

2. AZAM FC HAWEZI KUTUFIKIA TENA KWA SASA

"Azam hawezi kutufikia tena, mpinzani aliyebaki ni Yanga ambaye na yeye tunataka kumfunga na kumpita kwa alama sita. Ni mechi ambayo tunaitaka kweli kweli, kuanzia kwa mashabiki, benchi la ufundi, wachezaji na viongozi ndio hata hatulali."

"Tumewekeza zaidi kwenye kuwafurahisha mashabiki wetu, Jumapili ya Novemba 5, 2023 tunataka kuwafurahisha. Na anayeshinda mchezo huo ndio atatawala nchi hadi tukikutana tena."

"Mashabiki wetu tuzingatie misingi ya uungwana na ustaarabu, tujitahidi tushangilia na kutaniana kwa heshima ili kuepusha vurugu. Tuendeleze Utanzania kwa utu na upendo."

"Tumecheza mechi ngumu lakini mechi ya Jumapili ni ngumu kuliko zote hii ni kutokana na utani uliopo pamoja na ubora wa timu yao. Tunaona namna wachezaji wao wanajituma. Mechi yetu dhidi yao ni ngumu kweli kweli, mechi ya kipimo cha mpira wa nchi haiwezi kuwa nyepesi."

3. VIINGILIO SIMBA VS YANGA

"Ni mechi ambayo Wanasimba inabidi tujitoe muhanga ili kupata ushindi. Kila Mwanasimba ajue ana jukumu la kusaidia timu yake. Tukishinda siku hiyo shughuli itakuwa imeisha, itabaki shughuli ya kukamilisha ratiba ya msimu."

"Raha ya msiba waliaji wawe wengi, tunawaomba mashabiki wao waje uwanjani na wakae hadi mwishoni sio tukishawafunga wawahi kuondoka, wasubiri hadi mchezo uishe."

"Viingilio Mzunguko - Tsh. 5,000, Machungwa - Tsh. 10,000, VIP C - Tsh. 20,000, VIP B - Tsh. 30,000, VIP A - Tsh. 40,000 na Platinum - Tsh. 150,000."

4. TUTAINGIA KAMBINI KESHO KWA MECHI YA YANGA

"Kikosi kitaingia kambini kesho Jumanne, kwa kawaida mechi za ndani huwa tunaingia siku tatu kabla ya mchezo lakini hii tunawahi. Tumeutolea macho mchezo huu kuhakikisha tunapata ushindi."

"Kocha wao ameshakuja kwenye mechi tatu hadi sasa na leo tunatangaza kumkaribisha kwenye mazoezi yetu yatakayofanyika Mo Simba Arena. Tunamualika rasmi aje siku yoyote anayotaka."

"Sisi hatuna jambo dogo hivyo tutafanya hamasa, ni mchezo wetu, tutautangaza tutakavyo tunajua watu watakuja lakini lazima tuichangamshe. Tutakuwa na wiki ya mchakamchaka wa kuaga kwao aage atarudi Jumatatu ya Novemba 6, 2023."

"Siku ya Ijumaa tutakuwa na biryan la derby. Bado tunaangalia eneo la kufanyia."

5. MOSES PHIRI KUHAMIA YANGA

"Tetesi za Moses Phiri kuondoka kwenda Yanga SC au timu nyingine niwambie tu wataendelea kumtamani kama wanavyotamani wachezaji wengine. Moses ataondoka Simba siku tukiamua kuachana nae na siku hiyo siioni, hawatampata General hata siku moja."

"Kwanza Moses Phiri anaondokaje Simba. Simba ni sehemu ya wachezaji kutimiza malengo yao, wachezaji wetu ni matajiri, wanaishi maisha ya kifalme."

"Sio kila wanaokutana uwanjani kwamba ugomvi wao umeanzia hapo, kuna wengine wanatafutana tangu mtaani na wamekutana pale. Tuangalie namna ya kutoa taarifa ya haya matukio."

"Sisi kama Simba tunakemea hayo matukio, hata kama mna sababu zenu msije kugombania uwanjani maana inaleta picha tofauti, sio kitendo cha kufurahisha. Simba usivuke mipaka yako, Yanga usivuke mipaka yako. Tunalaani na tusingependa kuona tukio kama hilo linajirudia."

"Mpira wa Tanzania umejengwa katika #KariakooDerby ya Simba na Yanga, ni mechi ambayo imebeba kila kitu cha mpira wa nchi hii. Ni mechi yenye thamani kubwa."

"Mechi ya AFL hatukuuza tiketi zote, walizuia baadhi ya tiketi kwa sababu ya kiusalama, lakini mechi ya #KariakooDerby tutauza tiketi zote. Tunataka hadi Ijumaa ikiwezekana tiketi ziwe zimeisha na tunatamani mashabiki wengi tuwe wa Simba."

6. MGENI RASMI MECHI YA SIMBA NA YANGA

"Mgeni rasmi wa mchezo wa Jumapili Novemba 5, 2023 ni Kibu Denis Prosper."

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement