SIMBA Queens imeendeleza ubabe na kugawa dozi baada ya kuichapa JKT Queens mabao 2-0 Uwanja wa Azam Comlex, Chamazi ikiwa juzi tu imetoka kumchapa mtani wake Yanga Princess 3-1 na kusalia kileleni.

Mabao ya Simba yamefungwa na Aisha Mnunka dakika ya 5 akipokea pasi kutoka kwa Jentrix Shikangwa na kumfanya afikishe mabao 16 ikiwa tofauti ya bao moja na kinara Stumai Abdallah mwenye 17 na bao la pili likaongezwa baada ya JKT kujifunga kwa mpira wa faulo uliopigwa na Ruth Ingosi.

Kwa matokeo hayo yanaifanya Simba iendelee kusalia nafasi ya kwanza na pointi 37 ikijiweka katika nafasi nzuri ya kuchukua ubingwa msimu huu baada ya kupishana pointi tisa na mpinzani wake JKT mwenye 28.

Katika mechi tano ambazo Simba Queens imebakiza ikishinda tatu itafikisha pointi 46 ambazo haziwezi kufikiwa na JKT Queens hivyo itatangaza Ubingwa. JKT ikishinda mechi zake zote tano zilizobaki itafikisha pointi 43.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement