Miamba ya Soka Tanzania tayari imewajua wapinzani wao katika hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika (CAF).

Shirikisho la soka Afrika CAF limepanga droo ya hatua ya robo fainali ya michuano ya CAF Champions League msimu wa 2023/2024.

Wawakilishi wa Tanzania Simba na Yanga kila mmoja ataanzia nyumbani kutokana na kumaliza nafasi ya pili katika kundi lao na michezo ya mkondo wa kwanza itachezwa tarehe 29 na 30 March 2024 huku marudiano yakiwa ni April 5 na April 6 2024.

Simba SC wamepangwa kucheza dhidi ya Al Ahly ya Misri wakati watani zao wa jadi Yanga wamepangwa kucheza dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement