Ligi ya soka ya Africa (AFL) Ilizinduliwa Agosti 2022, Ligi Kuu ya Afrika sasa itajulikana kama Ligi ya Soka ya Afrika na, baada ya kucheleweshwa mara kadhaa, hatimaye itaanza mwishoni mwa Oktoba 2023.

Timu nane zitakazoshiriki Ligi ya Soka ya Afrika 2023 zimethibitishwa.

Timu moja imechaguliwa kutoka kwa kila ligi iliyo daraja la juu barani na Ligi Kuu ya Soka Afrika Kusini itawakilishwa na Mamelodi Sundowns.

Hiyo ina maana kwamba wababe wa jadi wa PSL, Kaizer Chiefs na Orlando Pirates wamekosa nafasi hiyo.

Walioungana na Mamelodi ni vigogo wa Misri Al Ahly, Wydad Casablanca ya Morocco, Esperance, TP Mazembe, Enyimba Football Club ya Nigeria, Simba SC kutoka Tanzania na Petro Atletico kutoka Angola.

Droo ya robo fainali ya Ligi ya Soka ya Afrika ilipangwa Septemba 2, ratiba imethibitishwa.


Robo fainali ya mkondo wa kwanza:

20/10/23 saa 15H00: Simba SC (Tanzania) vs Al Ahly (Misri)

21/10/23 saa 13H00: TP Mazembe (DR Congo) vs Esperance (Tunisia)

21/10/23 saa 15H30: Petro Atletico (Angola) vs Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini)

22/10/23 saa 18H00: Enyimba (Nigeria) vs Wydad Casablanca (Morocco)


Robo fainali ya mkondo wa pili:

24/10/23 saa 14H00: Al Ahly (Misri) vs Simba (Tanzania)

24/10/23 saa 17H00: Sundowns (Afrika Kusini) vs Petro Atletico (Angola)

25/10/23 saa 15H00: Esperance (Tunisia) vs TP Mazembe (DR Congo)

25/10/23 saa 18H00: Wydad Casablanca (Morocco) vs Enyimba (Nigeria)

Kwa mujibu wa taarifa, nusu fainali ya Ligi ya Soka ya Afrika itachezwa Oktoba 29 (mkono wa kwanza) na Novemba 1 (mkono wa pili).

Mechi ya kwanza ya fainali itafanyika Novemba 5, na marudiano yatachezwa siku sita baadaye Novemba 11.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement