Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amethibitisha kuwa klabu hiyo itatumia Uwanja wa CCM Jamhuri Morogoro kama uwanja wao wa nyumbani na itaanza na Prisons Machi 6, 2024.

Simba itatumia uwanja huo kwa mechi zake za nyumbani baada ya Uwanja wa Uhuru waliokuwa wakiutumia hapo awali kufungwa kwaajili ya maboresho.

Pia, Ahmed amezungumzia afya ya Willy Esomba Onana ambaye alikuwa majeruhi kwa muda kidogo.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement