Shirikisho la soka Tanzania TFF limetangaza tarehe za michezo ya Ngao ya Jamii mwaka huu, ambayo itachezwa mwanzoni mwa mwezi Agosti, 2024.

Michezo ya Ngao ya Jamii itachezwa kwa mfumo wa mtoano ili kupata timu mbili zitakazocheza fainali Agosti 11, 2024 katika uwanja utakaotangazwa baadae na TFF.

Michezo ya mtoano imepangwa kuchezwa kuanzia Agosti 8, 2024.

Kutokana na kanuni za michuano hii mshindi wa kwanza (Yanga) atacheza na mshindi wa tatu (Simba), huku Azam FC iliyomaliza nafasi ya pili itacheza dhidi ya mshidni wa nne Coastal Union.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement