Shirikisho la soka la Senegal (FSF) linataka kumuongeza mkataba Kocha Aliou Cissé hadi fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 nchini Morocco.

Cissé ambaye amekuwa ofisini tangu Machi 2015, ndiye Kocha aliyekaa muda mrefu zaidi katika historia ya Senegal. Mkataba wake wa sasa unamalizika mwishoni mwa Agosti. 

Licha ya kuondolewa kwa Senegal katika hatua ya 16 ya AFCON 2023, Rais wa FSF, Augustin Senghor, alisisitiza imani yake kwa Cissé. 

Ikiwa Cissé ataongeza mkataba wake, atapata fursa ya kucheza AFCON yake ya 5 kama kocha wa Senegal. Pia atalenga kushinda AFCON yake ya pili akiwa na timu ya taifa baada ya ushindi wao mwaka wa 2021.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement