SHIRIKISHO LA MPIRA ZFF LADHIBITISHA MAOMBI YA KUWA WENYEJI WA MICHUANO YA CECAFA 2024
SHIRIKISHO la Soka Zanzibar (ZFF), limethibitisha kukamilisha maombi kuwa mwenyeji wa mashindano ya CECAFA Senior Challenge 2024, yanayotarajiwa kufanyika Julai, mwaka
Mataifa washindi wa tenda hizo wanatarajiwa kutangazwa katika Mkutano Mkuu wa wa Cecafa utakaoafanyika Februari 23, 2025 jijini Mombasa, Kenya.
ZFF imefanya hivyo baada ya Cecafa kutangaza nafasi za kuwania kuandaa mashindano mengine matano yatakayofanyika mwaka 2024 ambayo ni Kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika 'Afcon' kwa wanaume chini ya miaka 17 na 20, (AFCONU-17 Boys qualifiers), na (AFCON U-20 Boys qualifiers), kuwania kufuzu Ligi ya Mabingwa Afrika kwa wanawake ngazi ya klabu (CAF Women's Champions League Zonal qualifiers), kuwania kushiriki michuano ya kutafuta Bingwa wa Shule za Afrika (Africa Schools Football Championships Zonal qualifiers), pamoja michuano ya Ubingwa wa CECAFA kwa Wanawake chini ya umri wa miaka 20 (CECAFA U-20 Girls Championship).
Wakati huo timu shiriki zilikuwa tisa, Uganda, Burundi, Djibouti, Eritrea, Kenya, Somalia, Sudan, Tanzania na Zanzibar.